Habari za Mastaa

Mkubwa Fella kajibu haya kuhusu ishu ya yule dada aliyedai kuitwa Dar na Dogo Aslay… #UHeard (Audio)

on

fella

Jana Soudy Brown kapiga stori na binti aliyedai kuwa Dogo Aslay alimwambia aje Dar ili wakutane na kuweza kumsaidia kupata kazi.

Leo Said Fella kasikika na kusema hao ni matapeli waliotumia jina la Dogo Aslay na ni vizuri watu wakawa makini na mitandao ya kijamii kwa kuwa watu wamekuwa wakitumia majina ya wasanii kufanya utapeli.

Amesema huyo si Dogo Aslay wa kweli bali ni mtu aliyetumia jina lake… Soudy Brown akaona amtafute tena yule dada toka Geita ambae aliongopewa na Aslay feki mtandaoni, kajitahidi kumwambia kwamba yule hakuwa Aslay lakini dada hata hakuelewa somo.. anaamini yule alikuwa Aslay na kwa sasa yuko South Africa.

U Heard iko hapa, story za Soudy Brown, Mkubwa Fella na yule msichana aliyetapeliwa ziko kwenye hii sauti hapa.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments