Habari za Mastaa

Mtayarishaji Tuesday Kihangala kajibu malalamiko ya kutowalipa Witness pamoja na mpenzi wake… #UHeard (Audio)

on

wt na ochu

Jana Witness alisikika kwenye U Heard, kwenye malalamiko yake ni kwamba alidai kampuni ya Tuesday Entertainment haijawalipa fedha zao za kufanya tamthilia  ya High Heels kwa miezi nane sasa na kutokana na makubaliano yao ilikuwa walipwe kiasi cha kama Milioni 10 hivi, yeye pamoja na mpenzi wake Ochu !!

Soudy Brown  amemcheki Mr. Chuz ambaye ndio mmiliki wa Kampuni hiyo, yeye amesema hakuna ukweli wowote juu ya stori hiyo, ila kilichopo ni kwamba Witness amekuwa haudhurii kazi ndio sababu iliyofanya asiwalipe fedha zao.

Mr. Chuz amesema kwa upande wa Ochu atalipwa pesa yake wakati wowote atakapokwenda kuchukua lakini Witness hawezi kumlipa kwa kuwa hajafanya kazi kama walivyokubaliana.

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments