Habari za Mastaa

Tundaman kamdhulumu dereva wa Bajaji? Imemfikia Soudy Brown hii …#UhearD JULY28

on

tundaa

Soudy Brown katafutwa na jamaa ambaye anadai kwamba ana deni na staa wa Bongo Fleva, Tunda Man… Huyo jamaa anadai walikubaliana ampeleke na kumrudisha kutoka Changanyikeni mpaka Lamada wakati akiendelea na mipango ya kushoot video ya Qaswida.

Amesema walikubaliana wamlipe 60,000 lakini baadaye akaanza kuzungushwa na kila akimpigia simu hapokei hadi baada ya wiki na kuahidi atamtumia lakini mpaka sasa hajamtumia.

Tundaman mwenyewe amesema alimwambia aje kuchukua lakini hakuja, na yeye hawezi kumdhulumu na yupo tayari kummalizia fedha yake iliyobaki ambayo ni 25,000.

Wasikilize hapa…

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments