Top Stories

Tofauti kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Marais wengine wa Kenya.

on

Screen Shot 2014-09-07 at 12.39.52 AMRipota wa TZA (millardayo.com na AyoTV) Kenya Julius Kepkoich anatiririka kwamba Uhuru Kenyatta ametajwa kama rais anayejitokeza kwa njia ya kipekee toka Kenya ianze kutawaliwa akiwa pia ni rais wa kwanza kenya kumiliki kiti kilichowahi kukaliwa na baba yake.

Tangu kutwaa madaraka Kenyatta amekua akifanya mambo yasiyo ya kawaida kwa Rais yeyote hasa hapa Afrika yeye ametajwa kua  anatumia sana mitandao ya kijamii kuwasiliana na watu, pia amewashangaza wengi kwa kutumia gari moja tu kwenye shughuli zake za kibinafsi.

Screen Shot 2014-09-07 at 12.40.04 AMKingine alichotajwa nacho ni kujichanganya na raia wengine wa kawaida kwenye maisha ya kawaida kabisa hata kununua karanga kwenye foleni ya magari, kujivinjari ufukweni Mombasa na wakenya tu wa kawaida.

 

Screen Shot 2014-09-07 at 12.39.45 AM

Wiki hii Rais Kenyatta anatufungia wiki kenya kwa picha za kipekee alizopost akiwa na magwanda ya kijeshi juu chini, ikasababisha iwe ni trend kwenye mitandao na kila mtu akaandika chakwake, mwingine military Swagg, ameamua kwenda somalia mwenyewe, the happiest Army officer na commander in chief na mengineo

Screen Shot 2014-09-07 at 12.39.37 AM

Screen Shot 2014-09-07 at 12.39.29 AMNi halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu na niko tayari kukutumia wakati wowote iwe usiku au mchana iwapo utakua umejiunga na mimi kwa kubonyeza hapa >>> twitter Insta FB

Tupia Comments