Habari za Mastaa

U Heard ya Novemba 27 iko hapa, Steve Nyerere amjibu Linex kuhusiana na gari analodai kudhulumiwa

on

IMG_4502U Heard ya jana alisikika Linex ambaye alilalamika kudhulumiwa pesa kiasi cha milioni 11 na Nyamihela, ambaye alikutanishwa na muigizaji Steve Nyerere ambapo Linex alisema lengo lake ilikuwa ni kununua gari na Steve alimkutanisha na huyo jamaa kwa ajili ya kufanya biashara hiyo.

Leo amesikika Steve Nyerere ambapo amesema yeye aliwakutanisha Linex na Nyamihela baada ya Linex kumwambia kwamba anahitaji kununua gari, lakini baada ya hapo hakuwa na mawasiliano tena na Linex.

Steve amesema Linex alimtafuta baada ya kushindwana na Nyamihela na kumlalamikia Steve kwamba Nyamihela kamdhulumu pesa ambayo alimpatia ili amuuzie gari, japo Steve amesema kiasi cha pesa alichopatiwa Nyamihela ni milioni tatu na alimrudishia milioni moja kati ya pesa hizo.

Kuisikiliza U Heard hiyo bonyeza play hapa chini.

Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments