Habari za Mastaa

U-HEARD: Shamsa Ford ameelezea kisa cha kupigwa ngumi

on

April 19, 2017 kupitia U heard ya XXL ya Clouds FM mtangazaji Soudy Brown ametuletea stori inayomuhusu staa wa Bongo movie Shamsa Ford ambaye amepata majeraha jichoni baada ya kupigwa.

Inadaiwa kuwa Shamsa alipata majeraha hayo baada ya kupigwa ngumi wakati anaamulia ugomvi wa mtumishi wake wa ndani ambaye alikuwa anazozana na mwanaume aliyemdhalilisha kwa kumshika mwili wake bila ridhaa yake.

Ili kujua undani wa tukio hilo, Soudy alipiga story na Shamsa ambaye alisema: >>>“House girl wangu alichokozwa na mwanaume, so wakawa wanagombana, nikaenda kuamulia basi, ngumi ikanipata. Nilipelekwa hospitali na mume wangu.” – Shamsa Ford.

Bonyeza Play hapa chini kusikiliza Full Story….

VIDEO: Taarifa za msiba wa Baba mzazi wa Belle 9 

Soma na hizi

Tupia Comments