Michezo

Hii ni good news kwa mwanasoka mwingine toka Tanzania…

on

Wakati idadi ya wachezaji wa kitanzania inazidi kuongezeka kucheza soka katika ligi kubwa Afrika au nchi yoyote ambayo soka lake lipo juu kuliko Tanzania ni dalili na ishara njema ya soka letu kukua.

Hii ni zamu ya kiungo wa Simba Uhuru Suleiman Mwambungu ambaye amejiunga na klabu ya Jomo Cosmos ya Afrika kusini.

Uhuru amejiunga na Jomo Cosmos iliyopanda daraja msimu huu na tunategemea kumuona akifanya vizuri ili aweze kuja kusaidia taifa. Licha ya muda wa mkataba wake kutotajwa ila inadaiwa Uhuru atakuwa analipwa kiasi cha d0la 5000/= ambayo ni zaidi ya Tsh millioni 9 kwa thamani ya dola kwa sasa.

Uhuru anakuwa mchezaji wa pili wa Tanzania kwa mwaka huu kuingia katika ligi kuu Afrika Kusini maarufu kama PSL baada ya Mrisho Ngassa kujiunga na klabu Free State ya Bethlehem Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka minne.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments