Habari za Mastaa

U Heard: Majibu ya Harmonize baada ya kudaiwa kuachana na Wolper

on

Kupitia XXL ya Clouds FM leo May 4, 2017 mtangazaji Soudy Brown ametuletea U heard ambayo inawahusu mastaa wa Bongo Fleva na Bongo Movie Harmonize na Jacqueline Wolper ambao wanadaiwa kuachana.

Inadaiwa pia kuwa staa Harmonize kutoka WCB amepata mchumba mpya raia wa Italia ambaye tayari ana ujauzito wake.

Baada ya Soudy kumpigia simu Wolper aliambiwa amuulize Harmonize ambaye naye alipoulizwa alikuwa na majibu haya:

“Kila kitu kinawezekena, hata Adam na Hawa walipotezana miaka kibao wakaja kuonana kwa bahati mbaya. Kuhusu kumpa mimba huyo mzungu, inaweza kuwa ni baraka maana pale WCB nimebakia mimi tu; Diamond, Ray Vanny na Rich Mavoko wana watoto.” – Harmonize.

Bonyeza Play kusikiliza Full Story hapa chini

EXCLUSIVE : “Natamani kufanya kazi na Alikiba” – Amanda

Soma na hizi

Tupia Comments