Habari za Mastaa

PICHA 4: Unahitaji Milioni 500 ili kumiliki daftari lenye ngoma za Lil Wayne

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ unaripoti kuwa kwa mtu yeyote mwenye uhitaji wa kumiliki daftari lililojaa ngoma za Rapper Lil Wayne basi anahitaji kuwa na shilingi milioni 500 za Kitanzania ili kulipata daftari hilo lenye mistari kadhaa. 

Inaelezwa kuwa daftari hilo lenye mistari ya Lil Wayne ambalo aliandika kuanzia mwaka 1999 kwa sasa lipo sokoni na linapigwa bei na kampuni ya Moments In Time na kutajwa kufikia dola za Kimarekani 250,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 586 za Kitanzania.

Inaripotiwa kuwa ndani ya daftari hilo kuna mistari ya ngoma kama “We On Fire” na “I Feel” kipindi hicho akiwa na kundi la Hot Boys akiwa na umri wa miaka 17.

Inaelezwa kuwa mmiliki wa daftari hilo kwa sasa ni kijana mmoja ambaye anadai kuwa alilikuta kwenye gari lililokuwa gereji wakati likimilikiwa na Cash Money Records, daftari hilo lilikuwa limelowa maji kutokana na mafuriko yaliyotokana na kimbunga Katrina ambapo vitu vyake vingi vilipata maafa kasoro boksi ambalo lilikuwa na daftari hilo.

ULIPIWA NA DC JOKATE ALIVYOSHINDWA KUJIZUIA NA KUSEREBUKA TAIFA? Bonyeza PLAY kutazama mwanzo mwisho.

Soma na hizi

Tupia Comments