Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Kamsisi Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi Leornad Mapinda (51) ameuwawa na Watu wasiojulikana kwa,kukatwa sehemu mbalimbali za mwili wake.
Mwenyekiti wa kamati ya Usalama Wilaya ya Mlele ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Alhaj Majid Mwanga amelaani kitendo hicho na kuagiza Jeshi la Polisi kuwasaka watuhumiwa.