DC wa Kisarawe Jokate Mwegelo ambaye alikuwa mwenye shughuli ya harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa shule ya bweni ya wasichana kwenye kampeni ya ‘Tokomeza Zero’ ametumia ukurasa wake wa instagram kumshukuru Pierre kwa kuhudhuria pamoja na kuchangia Tsh laki moja kwaajili ya ujenzi.
DC Jokate pia amempa Pierre dili katika mradi wa ujenzi wa shule hiyo ya bweni katika Wilaya ya Kisarawe ikiwa shule hiyo itahitaji madawati basi dili hilo amepewa Pierre kutokana na yeye kuwa muuzaji wa furnitures maeneo ya Keko jijini DSM kabla ya umaarufu.
“NIMERUDI!!Hakuna maneno Muhimu na Machache katika ustawi wa maisha ya Binadamu kama Tafadhali, Asante na Samahani.Katika Dhifa niliyoiandaa jana, nilialika watu wengi, Wanasiasa, Taasisi za Kiserikali, Mabalozi, Wafanyabiashara, Wajasiriamali, Wasanii, Wadau wa Burudani N.k.
Na Makusudio ya yote hayo wote tunayajua, ni kutafuta MOTISHA juu ya ELIMU ya Mtoto wa kike, Kisarawe na kote nchini”
“Na kwangu mimi na Wilaya nzima ya Kisarawe wote waliofika jana ni muhimu sana sana kwangu na kwetu. Kipekee kabisa nimshukuru @officialpiere_liquid wako watu maarufu wengi mno tuliowaalika lakini hawakufika. Ila wewe ulichukua muda wako kuhamamisha na kufika na zaidi ya hapo ukatoa mchango wa TSH LAKI MOJA!!! Hukuja kuuza sura tu!! Nasema ASANTE SANA. Wana Kisarawe tunakupenda na tunakukaribisha kuwekeza Kisarawe uanzishe hata mgahawa tutakusaidia kupata eneo. Lakini pia nimesikia ni mtengeneza mzuri sana wa furniture”
“Hii Shule tunayoenda kujenga inahitaji madawati Naomba tufanye kazi nawewe katika hii fursa. Tuangalie namna japo kidogo tukuwezeshe. Tunasema Karibu Kisarawe Ukae. Kisarawe Kunogile. Tunasema Samahani kwa kukwazika lakini zaidi Asante Sana kwa kushiriki kwenye #TokomezaZeroKisarawe#ElimuItabakiKuwaJuuKileleni#KisaraweMpya Ubarikiwe!!!!”
ULIPITWA NA MANENO YA WAZIRI KIGWANGALLA KUWA SAMBAMBA NA PIERRE ‘ANACHEKESHA’? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA.