Watoto watatu walionusurika kwenye ajali ya basi la wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent ambayo ilipoteza maisha ya wanafunzi 32, wanatarajia kurejea nchini August 18, 2017 baada ya kupatiwa matibabu Marekani.
Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu ambaye alikuwa mstari wa mbele kusimamia shughuli ya kuwasafirisha, amesema ratiba ya mapokezi itaanza mapema zaidi ambapo itakuwa saa Moja asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, ‘KIA’ ambapo Makamu wa Rais Samia Sulu Hassan atawaongoza Watanzania.
>>>”Watawasili tarehe 18, 2017 wiki hii wakiwa wanaletwa na ndege ile ile iliyowachukua na ratiba inaanza mapema kidogo saa moja asubuhi, wananchi na wanafamilia wanatarajiwa wawe wamefika uwanja wa KIA, Kutakuwa na viongozi mbalimbali na tunatarajia makamu wa Rais kuwa mgeni rasmi.” – Lazaro Nyalandu.
Watoto 3 majeruhi wa ajali ya basi la wanafunzi wa Lucky Vincent wanatarajia kuwasili Aug 18 baada ya kutibiwa Marekani. #MillardAyoUPDATES. pic.twitter.com/CtUJz82Ihy
— millard ayo (@millardayo) August 15, 2017
‘Waiuze soko la nje lakini zuio liko palepale’ – SERIKALI kuhusu pombe ya Viroba