Michezo

Cristiano Ronaldo kwenye rekodi mpya, kapiga goli la 700 Ukraine

on

Timu ya taifa ya Ureno usiku wa October 14 2019 walikuwa Ukraine kucheza mchezo wao wa kuwania kufuzu fainali za Euro 2020 dhidi ya Ukraine, mchezo ambao wengi walikuwa wakisubiri kwa hamu kumuona nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo akifunga goli lake la 700 katika maisha yake ya soka

Goli la penati la Cristiano Ronaldo aliloifungia Ureno dakika ya 72 kwa penati dhidi ya Ukraine katika kipigo cha 2-1 katika mchezo wa kuwania kufuzu Euro 2020, linamfanya Ronaldo atimize jumla ya magoli 700 katika maisha yake ya soka (Sporting magoli  5, Man United magoli 118, Real Madrid magoli 450, Juventus magoli  32 na Ureno akifunga magoli 95).

Hata hivyo Ureno mchezo huo walipoteza magoli ya Ukraine yakifungwa na Roman Yaremchuk dakika ya 6 na Andriy Yarmolenko dakika ya 27, hata hivyo Ureno wanatakiwa kujihakikishia wanapata matokeo mazuri katika michezo yao minne iliyosalia kwani wapo nafasi ya pili wakiwa na point 11 huku Ukraine akijiweka vizuri kwa kuwa kinara kwa point 19 ila amemzidi Ureno mchezo mmoja zaidi akicheza michezo saba.

Matokeo ya game za Euro 2020 zilizochezwa usiku wa October 14 2019.

VIDEO:AJIB BWANA MIPANGO !!! KAANZISHA MOVE NA KWENDA KUFUNGA

Soma na hizi

Tupia Comments