Michezo

Mtoto wa Eto’o kaitwa timu ya taifa kwa mara ya kwanza

on

Baada ya kumalizika kwa zama za utawala wa Samuel Eto’o katika kikosi cha timu ya taifa ya Cameroon, sasa ni zamu ya utawala wa mtoto wake wa kumzaa anayejulikana kwa jina la Etienne Eto’o ambaye kwa sasa ameitwa timu ya taifa ya Cameroon U-17.

Etienne Eto’o ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Cameroon U-17 kinachojiaandaa na michuano ya Kombe la Dunia U-17, Etienne hakuwa sehemu ya kikosi cha Cameroon kilichocheza fainali za AFCON U-17 na kufuzu nchini Tanzania ila kwa sasa kocha Thomas Libiih ameona umuhimu wa kumuongeza mchezaji huyo.

Mtoto wa Eto’o alikuwa na nafasi ya kuchagua kucheza timu ya taifa ya Hispania au Cameroon kutokana na kuwa na uraia wa nchi mbili  kwa sababu ya kuzaliwa Hispania ila ameamua kuchagua kuchezea Cameroon, Etienne alizaliwa August 13 2002 na anacheza Mallorca-u17 ya Hispania akiwa kama nahodha wa kikosi hicho.

VIDEO: Uamuzi wa Simba SC kuhusu kudaiwa kugoma kwa Mkude, Erasto, Chama na Gadiel

Soma na hizi

Tupia Comments