Habari za Mastaa

Usiyoyajua kuhusu staa aliyeigiza Movie ya ‘SARAFINA’

By

on

Huyu ndie Leleti Khumalo maarufu kama ‘Sarafina’ mzaliwa wa Afrika Kusini ambaye alizaliwa March 30,1970 na alipata umaarufu baada ya kuigiza filamu ya Sarafina mwaka 1992 na filamu hiyo kutambulika kimataifa hadi kumpatia tuzo mbalimbali.

Leleti Khumalo alivaa uhusika kwenye filamu ya Sarafina kama msichana  wa shule ambaye hakuogopa kupigania haki zake na kuwahamasisha wenzake kusimama katika maandamano dhidi ya ubaguzi wa rangi uliokuwa ukifanywa nchini Afrika Kusini.

Leleti Khumalo kwa sasa ana umri wa miaka 48 na anasumbuliwa na ugonjwa wa ngozi unaofahamika kwa jina la Vitiligo ambao umeathiri sehemu kubwa ya ngozi yake ikiwemo usoni na mikononi.

Kutokana na mahojiano mbalimbali aliyowahi kufanya na vipindi tofauti vya habari Leleti alisema kuwa kwa mujibu wa madaktari walimuambia kuwa endapo atafanya maamuzi ya kuzaa basi ugonjwa huo utaathiri sehemu kubwa ya ngozi yake, lakini Leleti hakujali hilo na aliamua kupata watoto.Kwa sasa Leleti ana watoto wawili mapacha aliozaa na mfanyabiashara Skhutazo Winston Khanyile .

Bonyeza PLAY hapa chini kusikiliza mwanzo mwisho kuhusiana na miasma ya sasa ya Leleti Khumalo ‘Sarafina’

Nay wa Mitego kafunguka baada ya kufika BASATA “Hatuwezi kufanya kwa kubomoa”

Soma na hizi

Tupia Comments