Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Alikiba ‘Wasafi nimewasikia ila Niko busy na Mofaya, Nitawadhamini’

on

Baada ya muimbaji Diamond Platnumz kumtaka Ali kiba kuwa miongoni mwa wasanii watakao perform kwenye tamasha la muziki la Wasafi Festival, siku ya leo November 7, 2018 muimbaji Alikiba ameamua kumjibu Diamond kwa kupitia ukurasa wake wa instagram.

Alikiba amelikataa ombi hilo kwa kutoa sababu ya kuwa hawezi kushiriki tamasha hilo kwa sababu atakuwa busy na uzinduaji wa kinywaji chake cha Mofaya na kusema kuwa atadhamini tamasha hilo ili kusukuma gurudumu la la maendeleo ya sanaa Nchini.

“Baada ya subra ya muda mrefu, hivi karibuni nitawatangazia bidhaa yetu pendwa ya Mofaya inapatikana wapi na kwa kiasi gani! Pamoja na shughuli rasmi ya kuizindua kitaani”

“Pia ndugu zangu #Wasafi tumepata salamu zenu, nashukuru kwa mualiko wenu, ila kwa bahati mbaya sitoweza kushiriki kwa sasa kutokana na majukumu ya kuzindua Mofaya katika nchi zingine. Hata hivyo tusingependa kuwaacha hivi hivi, tupo tayari kuwapa support ya kudhamini tamasha lenu kupitia”

#MofayaEnergyDrink ili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya sanaa yetu Tanzania na Africa . Management #RockstarAfrica yangu tutaendelea kuwasiliana nanyi tuweze kufanya hili jambo kubwa. #MofayaByAlikiba#KingKiba”

EXCLUSIVE: Mtanzania aliepambana na Chui mpaka akamuua

Soma na hizi

Tupia Comments