Serikali ya Uingereza imetangaza kuwa kuanzia alhamisi ijayo tarehe 27 mwezi huu, haitohitaji watu kuonyesha vyeti vya vipimo vya Uviko19, vyeti vya chanjo na wataacha kulazimisha matumizi ya barakoa mashuleni, madukani na sehemu za mikusanyiko.
Kwa Mujibu wa Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema watalegeza masharti mengine yaliyokuwa yamewekwa kwa ajili ya kupambana na janga la Uviko19.
Aidha Serikali hiyo imetangaza kuwa haitowataka watu kufanyia kazi Majumbani. Uamuzi huu unaanza mara moja.