Uingereza imesitisha baadhi ya mauzo ya silaha kwa Israel, ikisema kuna “hatari ya wazi” vifaa hivyo vinaweza kutumika kufanya ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa.
Waziri wa Mambo ya Nje David Lammy alisema Uingereza itasimamisha leseni 30 kati ya 350 za kuuza silaha kwa Israel, na kuathiri vifaa kama vile sehemu za ndege za kivita, helikopta na ndege zisizo na rubani.
Waziri wa Israel aliiambia BBC kwamba uamuzi huo ulituma “ujumbe usio sahihi” na “ulikuwa wa kukatisha tamaa”, lakini shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International UK lilisema kusimamishwa huko “ni hatua ndogo mno”.
Lammy alisema Uingereza iliendelea kuunga mkono haki ya Israel ya kujilinda, na hii hailingani na vikwazo vya silaha.