Habari za Mastaa

“Wote ni wajukuu zangu” – Mama Diamond baada ya Hamisa kujifungua mtoto

on

Siku moja baada ya Mwanamitindo Hamisa Mobeto kujifungua mtoto wa kiume na story zikisambaa kuwa mtoto huyo ni mwimbaji staa wa Bongofleva Diamond Platnumz ingawa wenyewe wanazikanusha, sasa leo mama mzazi na dada wa Diamond wamefunguka.

Wakiongea kwenye na Soudy Brown kwenye U HEARD ya XXXL ya Clouds FM baada ya kuendelea kusambaa kwa taarifa hizo nao walifunguka.

>>>”Hamisa rafiki yangu siyo wifi yangu lazima niwe na furaha kwa sababu kajifungua salama. Wewe ulikuwa unataka nifanyeje? Hizo habari za Diamond mimi sizijui. Niulize mambo yangu. –  Esmaplatnumz

“Wewe unanitafuta nini Soudy? Naumwa kifua. Watoto wote ni wajukuu zangu hata wewe mtoto wako ukizaa mjukuu wangu. Wewe mwenyewe mwanangu, mtoto ukizaa mjukuu wangu. Wewe ni shushushu mbona hujafika Hospitali kumuona? Walioniona nimeenda Hospital waambie wakuhadithie vizuri. Mimi namuombea maisha mema alee mtoto wake vizuri kwa amani na furaha.” – Mama Diamond

Bonyeza Play hapa chini kusiliza FullStory..

GOOD NEWS: Hamisa Mobeto amepata mtoto wa kiume

Soma na hizi

Tupia Comments