Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Duh!! Lil Kim amkana Nicki Minaj, asema hamjui

on

Rapper mkongwe wa kike Lil Kim anayetikisa kwenye game ya Hip Hop Marekani amejibu swali aliloulizwa juu rapper wenzie wa kike  Cardi B na Nicki Minaj na kusema kuwa hamfahamu Nicki Minaj bali anafurahia kile anachofanya Cardi B.

Inadaiwa kuwa Lil Kim na Nicki Minaj hawako sawa tokea miaka kadhaa iliyopita na hivyo wote wawili walishawahi kukanana na kuongeleana vibaya kupitia mahojiano tofauti ambayo walishawahi kufanya, Lil Kim aliwahi kumuita Nicki Minaj nyoka kwenye moja ya mahojiano aliyofanya mwaka 2017.

Lil Kim amesema “Huyo mwingine simfahamu lakini Cardi B ni mwanangu sana na siwezi kusubiri yeye kupata mtoto, Cardi B nakupenda”

Jay Moe, Kuhusu Mahusiano yake, Na kwa nini hataki mtoto kwa sasa?

Soma na hizi

Tupia Comments