Inaripotiwa kuwa familia ya marehemu Nipsey Hussle imethibitisha kuwa mwili wa mpendwa wao utaagwa siku ya Alhamis April 11,2019 katika ukumbi wa Staples Center mjini Los Angeles Marekani.
Inaelezwa kuwa ukumbi huo una uwezo wa kubeba jumla ya watu 21,000 na shughuli za kuuga mwili huo zitaanza mapema asubuhi huku taarifa nyingine zikiripoti kuwa tiketi zimeanza kuuzwa mtandaoni kwa ajili ya kuingia eneo hilo na wamiliki wa tiketi pekee ndio watapata nafasi ya kuingia.
Ukumbi huo ulitumika kuuaga mwili wa mfalme wa Pop duniani Marehemu Michael Jackson mwaka 2009. Nipsey alifariki March 31,2019 baada ya kupigwa risasi nje ya duka lake ‘The Marathon Clothing” mjini Los Angeles.
VIDEO: ‘MIMI NA VANESSA HAKUNA TATIZO LOLOTE TUKO SAWA’ – JUX