Habari za Mastaa

Kesi ya unyanyasaji wa kingono inayomuandama R.Kelly yazidi kufukuliwa

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa waendesha mashtaka wa Mji wa Illinois watakaa kuanzia mwezi ujao kuzungumza na mashahidi wanaodai R. Kelly aliwahi kufanya kosa la kuwasafirisha wasichana wadogo na kuwatumia kingono.

Inaelezwa kuwa mashahidi hao watazipitia tiketi za ndege pamoja na vyumba vya hoteli alizowahi kuwafikishia wasichana hao wadogo pia ikiwemo kuzikusanya emails pamoja na meseji za kawaida ambazo zinaonyesha namna alivyokuwa akiweka mitego ya kuwanasa ili kuwasafirisha.

Inaelezwa kuwa R. Kelly akiwa bado anapambana na mashtaka 10 ya unyanyasaji wa kingono  siku ya May 7,2019  aliripoti Mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi wa video za ngono ambazo ziliwasilishwa na wanasheria kutoka kwa wasamaria wema.

VIDEO: JUMBA LA KIFAHARI LA REGINALD MENGI MACHAME

Soma na hizi

Tupia Comments