Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Imefichuka !!! Tyga aliwahi kumuoa baby mama wa Tristan Thompson

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umetoa taarifa kuwa Rapper Tyga aliwahi kufunga ndoa ya siri kipindi cha tisa nyuma, ambapo inaripotiwa kuwa ilikuwa September 2010 na alimuoa mwanamitindo Jordan Craig ambaye ni mzazi mwenza na Mchezaji wa mpira wa kikapu Tristan Thompson.

Inaelezwa kuwa mwanamitindo huyo alibahatika kupata mtoto wa kiume pamoja na Tristan Thompson 2016, huku taarifa nyingine zikiripotiwa kuwa Tristan alimsaliti mpenzi wake huyo akiwa mjamzito na kuanzisha mahusiano mapya na Khloe Kardashian ambaye pia baadae walibahatika kupata mtoto wa kike ambaye ni True Thompson. 

Fahamu kuwa Tyga aliwahi kuwa mapenzini na Kylie Jenner 2014-2016 baada ya kuachana na Blac Chyna ambaye walipata mtoto wa kiume Kairo, baadae Chyna alianzisha mahusiano na Rob Kardashian na kuzaa naye mtoto mmoja Dream Kardashian.

Baada ya TMZ kuripoti taarifa hizi mashabiki mbalimbali wamekuwa wakitoa comments zao kuhusiana na mzunguko wa familia hiyo ya ‘Kardashians’ ambavyo umekuwa ukienda kwenye swala zima la mahusiano ya kimapenzi.

VIDEO: ULIPITWA NA HII YA CHUCHU HANSY KUMTOLEA POVU RAY KIGOSI NA KUMUITA “BABA MWENYE JEURI”? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUATAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments