Tanzania imeendelea kupata mafanikio makubwa katika kuimarisha shughuli za uhifadhi kwa kutokomeza ujangili wa Wanyamapori, Biashara haramu ya nyara, mazao ya misitu na uvamizi wa maeneo yaliyohifadhiwa.
Wizara ya Maliasili na Utalii imesema kuwa eneo la ulinzi na usimamizi wa rasilimali za Wanyamapori, Misitu na Malikale limeendelea kupata matokeo chanya ndani ya kipindi cha miaka 60 ya uhuru kutokana na nguvu kubwa na mikakati madhubuti iliyowekwa katika kuhakikisha rasilimali zilizopo zinawanufaisha Watanzania.
Aidha, kupungua kwa Ujangili nchini kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na kuanzishwa kwa Jeshi la Uhifadhi wa Wanyamapori na Misitu ambalo limafanya kazi kubwa ya kutokomeza ujangili wa Wanyamapori na kuendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo ya Hifadhi nchini.
Chini ya Kauli mbiu Isemayo Tumerithishwa, Tuwarithishe, Jeshi hili limesaidia kuimarisha ulinzi na kuidhibiti vikundi vya uhalifu dhidi ya Wanyamapori kama tembo, faru, twiga na wengine waliopo katika hifadhi mbalimbali za Taifa.