Wakati ujenzi wa mradi wa majengo mapya ya ya kisasa ya makazi ukiendelea katika eneo la Nungwi Mashariki mjini Zanzibar, waendelezaji wanawakaribisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kwenye mradi huo wenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani milioni 100 (zaidi ya 236bn/-).
Kwa uwekezaji wa awali wa dola za Kimarekani 50,000 tu (118m/-), mwekezaji anaweza kuwa mmiliki wa mradi mkubwa wa The Ocean Pearl Zanzibar, unaotarajiwa kuwa wa aina yake visiwani baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza mwezi Januari 2025.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa na waendelezaji wa mradi huo, Squid Limited Zanzibar, Mkurugenzi Mtandaji wa kampuni hiyo, George Alexandru, alisema ujenzi wa madi ulianza Desemba 2022 kwa uchimbaji wa eneo hilo na kwamba awamu ya kwanza itakua na nyumba 238.
Mradi huo ambao umesajiliwa na Mamlaka ya Uwekezaji na Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) na kuthibitishwa kuwa na thamani ya dola za Kimarekani milioni 105 ambao unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 36, sasa unawakaribisha wezesha Wazanzibari na wasio Wazanzibari kununua nyumba hizo za kifahari.
Kwa mujibu wa marekbisho namba 10 ya Zanzibar Condominium Act ya 2010, baada ya ununuzi uliofanikiwa, mnunuzi atapewa hati ya umiliki ya kukodisha kwa miaka 99. Muda wa kukodisha kwa kawaida hutolewa kwa awamu za miaka 33 kila moja.
Wale wanaowekeza katika mradi huo ya kifahari watanufaika ka punguzo la kodi kama wakazi na makadirio ya kupata faida ya uwekezaji ya asilimia 12 kila mwaka huku malipo ya faida yakitegemewa kuanza kupatikana baada ya miaka saba, kwa mujibu wa mwendelezaji wa mradi huo.
“Baada ya kuwekeza katika The Ocean Pearl Zanzibar, iwe kwenye majengo ya studio, duplex au villa zakifahari, mwekezaji ana hiari ya kuikodisha kama nyumba ya mapumziko ya sikukuu au likizo au makazi ambayo itasimamiwa na kampuni mahususi ya kutoa huduma za ukarimu,” mkurugenzi mtendaji huyo alisema.
Mradi huo pia unatoa mchanganyiko wa kipekee wa huduma za bwawa la kuogelea, fukwe za bahari, chakula, na safari kwenye visiwa vya karibu, historia na utamaduni. Mradi wenye hadhi ya nyota tano utakuwa na huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na migahawa kadhaa, baa pamoja na baa kwenye gati, klabu ya usiku, duka la chokoleti, spa na eneo la mazoezi (gym), na mabwawa ya kuogelea.
“Tumeshirikiana na mbunifu mashuhuri, ASCO Construction and PVP Hospitality GmbH, kama mshauri wa kutekeleza mradi huo na tutatumia teknolojia endelevu za kutunza mazingira,” aliongeza Alexandru.
Awamu ya kwanza ya mradi inajengwa kwenye eneo la zaidi ya mita za mraba 130,000 itakayojumuisha kituo cha biashara wakati eneo kubwa litakuwa maalum kwa mabwawa ya kawaida na bustani huku ujenzi wa eneo la kutua helikopta unatarajiwa kuwezesha kufikika kwa anga, aliongeza.
Pamoja na usanifu wa hali ya juu, samani na matumuzi ya teknolojia endelevu, mradi huo utakuwa na uwiano mdogo wa matumizi ya ardhi wa asilimia 35 na unatarajiwa kuwa moja ya vituo bora vya michezo ya kuogelea.