Serikali imesema ujenzi wa Daraja jipya la Wami lenye urefu wa mita 513.5 na barabara za maingilio (KM 3.8), unatarajiwa kuandika historia kubwa kwa kukamilika kabla ya muda uliopangwa kwenye mkataba.
Ujenzi huu ulioanza mwezi Oktoba, 2018 unatarajiwa kukamilika mapema ifikapo mwezi Julai, 2022 badala ya mwezi Novemba kama ilivyo kwa mujibu wa mkataba wake.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, wakati akishuhudia ukamilikaji wa sehemu ya kupita magari (deck) kwenye daraja hilo jipya ambalo ujenzi wake umefikia 77% “Hii ni hatua kubwa sana kwa Daraja la aina hii, nimejionea linaendelea vizuri na naamini kutokana na kasi aliyonayo mkandarasi kwa hakika daraja hili litakamilika kabla ya muda” Prof. Mbarawa”
MAPYA YAIBUKA URUSI YATOA ONYO KALI KWA MAREKANI KUISAIDIA SILAHA UKRAINE