AyoTV

Ujerumani mkikutwa zaidi ya wawili na hamuishi nyumba moja faini Tsh laki 7

on

Mtanzania Emily Mgeta anayecheza soka katika club ya SV Endingen inayoshiriki Ligi daraja la tano nchini Ujerumani (Oberliga) amezungumza na AyoTV kwa njia ya simu  kutokea Ujerumani na kueleza mambo mbalimbali kuhusiana na hali yake ya sasa huko.

Emily yupo katika mji wa Freinburg na amekubali kueleza kila kitu, vipi maisha yapojea kwa upande wao huko wakati huu wa corona, Emily amekiri kuwa kwa Ujerumani hakuna Lock Down ya watu kutotoka nje ila imeruhusiwa watu kuongozana wawili na wakizidi hapo basi wawe watu wa nyumba au familia moja.

Kama mkikutwa nje watu zaidi ya wawili na sio kutoka familia moja basi mtapigwa faini ya kiasi kinachofikia Tsh laki 7, hiyo ikiwa sehemu ya faini na mbinu ya kujikinga na corona kwa upande mwingine wao wameruhusiwa kufanya mazoezi kama kawaida ila kwa makundi.

VIDEO: MBRAZIL WA SIMBA AFUNGA NDOA NA EDUARDA FRANCA

 

Soma na hizi

Tupia Comments