Michezo

Huyu ndio nahodha mpya wa timu ya taifa ya Ujerumani

on

iMiezi miwili baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia, huku timu ya taifa ya Ujerumani ikitwaa ubingwa wa dunia, nahodha wa timu hiyo Philip Lahm alifikia uamuzi wa kujiuzulu kuichezea timu hiyo na hivyo kuacha wazi nafasi ya unahodha kwenye timu hiyo,

Leo hii wiki kadhaa baada ya Lahm kujiuzulu, kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Low amemteua nahodha mpya wa timu hiyo.

Kiungo wa FC Bayern Munich  Bastian Schweinsteiger ndio amerithi nafasi iliyoachwa wazi na Philip Lahm.

Bastian mwenye miaka 30 ameshaichezea Ujerumani kwenye mechi zaidi ya 100 tangu alipoanza rasmi kuitumikia timu hiyo mwaka 2004.

Manuel Neur pia ameteuliwa kuwa nahodha msaidizi wa Ujerumani.

Tupia Comments