Muigizaji Shamsa Ford ameacha maswali mtandaoni hii ni baada ya kupost picha kupitia ukurasa wake wa instagram ikimuonyesha kuwa na jeraha usoni karibu na jicho na kusema kuwa wachunaji ndio huthaminiwa.
Caption aliyoiandika Shamsa Ford kupitia ukurasa wake wa instagram wengi wameihusisha kuwa huenda kuna jambo linaendelea katika ndoa yake pamoja na mume wake mfanyabiashara maarufu Chid Mapenzi
“Wanawake ambao tuna mapenzi ya dhati ndo huwa tunaonewa sana.Wanawake ambao huwa tunaishi maisha ya uhalisia kutokana na mifuko ya wanaume zetu ndo tunaonewa na kuonekana washamba.Lakini wale wanawake wachunaji ndo huwa wanapewa kipaumbele na kuthaminiwa” .
“Sielewi wanaume huwa wanataka nn kutoka kwa wanawake.Tunapigwa,tunasemwa vibaya,tunaonewa ,tunabeba mizigo mikubwa lakini mwisho wa siku bado unafuta machozi na kusema ALHAMDULILAH .Nyie wanaume huwa mnataka nini?🙌🙌 …”
Irene Uwoya “Mungu nisamehe naenda kuiba mwanaume wa mtu”