Mwimbaji mkongwe Oliver Mtukudzi amepumzishwa rasmi katika nyumba yake ya milele Jumapili ya January 27,2019 katika kijiji cha Madziwa kilichopo Kaskazini mwa Mji Mkuu wa Harare nchini Zimbabwe.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa alimpa heshima Oliver Mtukudzi ya kuwa Shujaa wa Taifa hilo siku ya Jumamosi January 26,2019 ambapo waombelezaji toka maeneo mbalimbali ya Zimbabwe walihudhuria shughuli ya kutoa heshima za mwisho katika Uwanja wa Taifa Mjini Harare.
Marehemu Oliver Mtukudzi alifariki January 23,2019 katika hospitali ya Avenues Clinic mjini Harare baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu.
IRENE UWOYA “Mimi na Dogo Janja tumeshindwana, nina mtu wangu akioa nitaenda”