Inaripotiwa kuwa muigizaji na mwanamitindo Kim Porter amefariki dunia usiku wa November 15,2018 baada ya kukutwa amefariki nyumbani kwake mjini Los Angeles Marekani.
Kim Porte ambaye ni mama wa watoto wanne aliozaa na Rapper P Diddy amefariki akiwa na umri wa miaka 47 na imeelezwa kuwa amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa homa ya mapafu (Pneumonia) kwa zaidi ya siku saba.
Kim Porte pamoja na P Diddy walibahatika kupata watoto watatu Christian Casey Combs, Jessie James Combs na D’Lila Star Combs na kuelezwa kuwa uhusiano wao ulidumu kwa miaka 13 ambapo walianza mahusiano mwaka 1994 na kuachana rasmi mwaka 2007.
KAULI YA KWANZA YA ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’ TOKEA AMALIZE KIFUNGO CHAKE