Habari za Mastaa

Chris Brown afunguliwa shtaka jipya ndani ya kesi ya ubakaji

on

Kwa mujibu wa mtandao wa The Blast umeripoti kuwa mwimbaji Chris Brown ameshtakiwa kutotoa taarifa kamili kwa mwanamke anayedai kumbaka nyumbani kwake mjini Los Angeles miezi kadhaa iliyopita baada ya mwanamke huyo kumfungulia shtaka la ubakaji.

Inaelezwa kwa mujibu wa nyaraka za Mahakama mwanamke huyo Jane Doe alifungua file lenye maswali  na kuitaka Mahakama kumuuliza Chris Brown kuhusu namba za simu alizokuwa akizitumia tokea tukio hilo February 2017 mpaka sasa kutokana na yeye kushindwa kupata jibu baada ya CB kumjibu kuwa ni swala binafsi na swali hilo halihusiani na kesi inayoendelea.

Inaripotiwa kuwa Mwimbaji huyo amezidi kukana shtaka hilo la ubakaji na kusema hakuna kitu kilichotokea nyumbani kwako huku Jane Doe akiamini kuwa endapo CB atakabidhi namba alizokuwa akitumia basi kutakua na ushahidi wa kutosha na amedai kuwa CB amekabidhi taarifa nusu.

Inaripotiwa kuwa Jane Doe alijikuta nyumbani kwa Chris Brown February,2017 baada ya kutoka kwenye kumbi za starehe na kudai kuwa CB alimlewesha na dawa za kulevya aina ya Cocaine, Marijuana na baadae kudai kuwa alifanyiwa kitendo cha ubakaji.

VIDEO: MABIBI NA MABWANA MISS IFM 2019 KAPATIKANA, KAZUNGUMZA HAYA

Soma na hizi

Tupia Comments