Habari za Mastaa

Wananchi Kenya walivyokasirishwa na picha ya Jaguar kwenye Range Rover Sport Mpya !!!

on

Moja kati ya stori zilizochukua headlines kwenye social network ni pamoja na stori ya Staa wa muziki nchini Kenya Jaguar, baada ya kuonekana akiwa na gari lake jipya aina ya Range Rover Sport, baadhi ya wananchi wameoneshwa kukasirishwa na hilo.

Jaguar alipost picha mtandaoni akiwa karibu na Range Rover Sport mpya, licha ya kuwa hajasema chochote kuhusiana na gari hiyo kama ni yake amenunua au alikuwa anapita karibu ya gari hilo lakini baadhi ya wananchi  wamemkosoa na wengine kumpongeza kwa mafanikio.

Ikumbukwe Jaguar ni Mbunge wa jimbo la Starehe sasa baadhi ya watu kuona amepost picha hiyo wameandika comment hizi “Inaumiza kuona wewe tuliekutegemea kutuwezesha kununua kilo ya unga kutufanya tusiijue kesho yetu Jaguar Wakenya wengi hawawezi kumiliki Range sisi tunahitaji tu NHIF”>>Danny Mkimzi

“Wewe sio kiongozi tuliyekuchagua tuone unapiga hatua wewe acha kupost vitu facebook na uanze kufanya kazi kwa watu wako waliyokuchagua kuwa kiongozi wao”>>>Evans Yatich

Meneja wa Diamond kauliza “Kumbe tatizo ni kumpoteza huyu kijana?

 

Soma na hizi

Tupia Comments