June 2, 2017 Mahakama Kuu Uganda imeomba Kaburi la Mfanyabiashara maarufu nchini humo Ivan Ssemwanga ‘Don’ libomolewe kisha zitolewe fedha zilizomwagwa na Kundi la Rich Gang wakati wa mazishi yake May 31, 2017.
Hatua hiyo inakuja baada ya Benki Kuu ya Uganda kutoa tamko kuvitaka Vyombo vya Dola kuwachukulia hatua waliotupa hela kwenye kaburi la Ivan Don ikiwa ni siku tatu baada ya mazishi ya Mfanyabiashara huyo maarufu.
Nakala ya Mahakama Kuu Uganda ikionesha ombi la kutaka kaburi la Ivan Ssemwanga libomolewe na kutolewa pesa zilizomwagwa wakati wa mazishi. pic.twitter.com/xm4lK2YjXP
— millardayo (@millardayo) June 2, 2017
FAHAMU kuhusu mambo matano yaliyojitokeza kwenye msiba wa Ivan The Don…yako hapa kwenye hii video. Bonyeza PLAY kutazama.