Bunge la 11 limeendelea Dodoma, na leo May 17 2016 ilikuwa ni zamu ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuwasilisha hotuba yake pamoja na kuomba kupitishiwa bajeti yake ijayo. Kazi imefanywa na Waziri wake Makame Mbarawa ambaye ameanza na kuzitoa changamoto za Wizara…
>>‘Katika utekelezaji wa majukumu yake Wizara inakabiliwa na changamoto mbalimbali, changamoto hizo ni pamoja na upungufu wa fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo, uzidishaji wa uzito wa magari ya mizigo unaosababisha uharibifu wa barabara‘
‘Msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam, uvamizi wa maeneo ya Hifadhi ya Barabara na Reli, kujenga uwezo wa Makandarasi wazalendo katika kutekeleza miradi ya maendeleo, ajali za barabarani, wizi wa miundombinu ya uchukuzi kutokana na biashara ya chuma chakavu n.k’
Mwisho Waziri Mbarawa akaomba fedha…>>>’Katika mwaka 2016/2017, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 4,895,279,317,500.00’. Kati ya fedha hizo, Shilingi 2,212,141,496,500.00 ni kwaajili ya Sekta ya ujenzi‘
‘Shilingi 2,587,333,762,000.00 ni kwa ajili ya Sekta ya Uchukuzi na Shilingi 95,804,059,000.00 ni kwa ajili ya Sekta ya Mawasiliano ‘
ULIIKOSA HII UTANI WA MASANJA AKIMPA RAIS MAGUFULI STYLE MPYA YA KUTUMBUA MAJIPU?
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE