Mix

Dereva alishika simu kwa sekunde 6 tu ikasababisha ahukumiwe miaka 10 jela

on

Tomasz Kroker alikua anaendesha Lori na kilichofanya ahukumiwe miaka kumi jela miezi miwili iliyopita ni uzembe alioufanya kushika simu yake ya mkononi ili abadili muziki ambapo akiwa kwenye hizo sekunde akasababisha ajali iliyosababisha vifo.

Kwenye hizo sekunde zisizozidi 10 wakati ametazama pembeni alikuja kushtuka yuko spidi na gari lake likayagonga magari mengine mbele yake na kuua mama na watoto watatu aliokua nao ambapo video ya tukio ilipatikana kupitia camera zilizo kwenye Lori hilo.

Ni tukio lililotokea Uingereza na Familia hiyo haikuridhika na adhabu ya miaka 10 jela aliyopewa Dereva huyo wakiamini ni ndogo, unaweza kutazama video yenyewe hapa chini na naamini itakufanya uwe makini barabarani kuanzia leo mtu wangu.

ULIPITWA? Bonyeza play hapa chini kumsikiliza Mfungwa Mtanzania aliyeibia simu Gerezani China na kumpigia simu Millard Ayo kumueleza yote ya Gerezani na kosa lenyewe

Soma na hizi

Tupia Comments