AyoTV

VIDEO: Sababu za UKAWA kususia bunge leo? wanayataka haya…

on

Bunge la 11 limeendelea tena April 22 2016, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipata nafasi ya kuwasilisha hotuba yake ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2016/2017
Baadae vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wametangaza kususia kuchangia hotuba ya Waziri Mkuu ndani ya bunge hadi pale Serikali itakaporekebisha vipengele vinavyo bana uhuru wa bunge kama vile kuruhusu urushwaji wa matangazo ya moja kwa moja na vyombo vingine kurekodi bila vizuizi.

Akiongea na Waandishi wa habari nje ya bunge, Dodoma Kiongozi wa upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesema ‘Hatutashiriki mjadala wa kibunge hadi tutakapopata rejea mpya ya muundo wa Serikali, Pili tatizo la bajeti za Serikali kufanywa kinyume cha sheria, n Serikali yenyewe inakiri tatizo hili‘ ;-Freeman Mbowe

Mwisho kabisa lazima muelewe, Bunge ni chombo cha Umma, sio mali ya mtu yoyote, tunapokuwa katika Bunge, kazi zinafanyika ndani ya Bunge na nje ya Bunge, kuna nia ya kuzuia mjadala unaojadili madhambi yanayofanyika katika Serikali yetu‘ ;Freeman Mbowe

Kama Serikali ya Rais Magufuli inajiamini, iruhusu mjadala huu uwe wa wazi na wa haki, sisi tunataka tumsaidie Rais kwasababu yeye amesema anataka Serikali ya uwazi, aturuhusu sisi tuielezee dunia madhara yaliyofanyika katika Serikali ya Nne na ya Tano ambayo huwenda kuna mengine hayajui‘ ;-Freeman Mbowe

Ilikupita hii Video ya Diamond Platnumz, Mrisho Mpoto Walivyotajwa Bungeni? 

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments