AyoTV

Ukali wa DC Jokate alivyoagiza watumishi wa Tanesco kupelekwa rumande ‘Sina huruma’

on

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Mh. Jokate Mwegelo amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za TANESCO wilayani humo na kukutana na malalamiko lukuki kutoka kwa Wananchi waliofika katika ofisi hizo, wakidai kucheleweshwa kwa uwekwaji umeme majumbani mwao, ikiwemo kero ya kukatika kwa umeme na hivyo kusababisha hasara kubwa kila uchwao kwa vyombo vinavyotumia nishati hiyo.

Mh. Jokate ameagiza kuswekwa rumande kwa baadhi ya watendaji wa idara hiyo, huku akiutaka uongozi kuhakikisha inatatua kero inayowakabili wananchi haraka iwezekanavyo.

Tupia Comments