Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mwanahamisi Munkunda amewataka wamiliki wa Bar zote wilayani humo kuacha tabia ya kutumia maeneo ya barabara “service road” kama sehemu ya biashara zao.
DC Munkunda ametoa kauli hiyo wakati akifanya usafi maeneo ya Buza wilayani humo ambapo amesema;
“Niwaambie ndugu zangu upo uchafu wa aina mbalimbali hapa Buza kuna uchafu wa aina nyingi ikiwemo kelele, watu mmefungua Bar bubu kwenye mitaa, mnapiga miziki mpaka saa 6 usiku wa manane,”- DC Temeke
“nikuombe Afisa Afya na nikuelekeze, Bar zote ambazo zilikuwa kama duka halafu ikifika saa 12 wanapanga viti mpaka barabarani kwenye Service Road, Katibu wa chama mtusaidie kwa sababu jioni watu wanageuza zile service road tena ndio Bar zao, lakini na kupiga miziki muda ambao hauruhusiwi,
“mnatengeneza kero kwa watu wanaotoka kutafuta Pesa wanarudi nyumbani wanakutana na kadhia ya kelele, kama eneo hilo matumizi yake sio biashara niwaombe sana na kama eneo hilo matumizi yake ni biashara fanya kiustaarabu,- DC Temeke