Top Stories

Ukali wa Rais Samia “Aibu askari kuchukua rushwa/kuna clip nimerushiwa kutoka Ulaya” (Video+)

on

Ni Agosti 25, 2021 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amehudhuria ufunguzi wa kikao cha maafisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi na makamanda wa Polisi wa mikoa/vikosi Dar es Salaam.
“Kwa upande mwingine Mwanadamu ni mwanadamu na ana uhuru wake naomba mkae na wadau wengine muangalie uwezekano wa kurekebisha sheria ya kumuweka mtu mahabusu”- Rais Samia
“Tuko hapa kuhudumia watu na si kudidimiza watu, ni aibu kuona kwenye simu zetu tunarushiwa clip Askari wa Jeshi la Polisi anakubaliana na Raia achukue rushwa”- Rais Samia
“Hasa Jeshi la Traffic huko upande wa Traffic na hawajui kwamba maendeleo ya Teknolojia haya, mtu aliekuwemo ndani ya gari anamrekodi kwa kalamu tu na wala sio hata simu, kwahiyo naomba mkayaangalie hayo muende mkayashughulikie tuondoe hiyo aibu”- Rais Samia

RAIS SAMIA AFUNGUKA “BAADHI YENU MNASHTUMIWA KWA KUTOFANYA HAKI/KESI ZA KUBAMBIKIZWA/UPELELEZI

Soma na hizi

Tupia Comments