Top Stories

Hizi ndio sababu za CUF kutoshiriki Mkutano wa UKAWA Dar es Salaam…

on

CJ5Ve-hVAAANFSN

Ziko stori nyingi toka jana mitandaoni, wapo waliopata taarifa pia kwamba chama cha CUF kimejitoa kwenye Umoja wa UKAWA, lakini hakuna msemaji rasmi aliyezungumzia ishu hiyo.

UKAWA jana walikutana na Colosseum Hotel Dar, katika moja ya post zilizowekwa kwenye Ukurasa wa @Twitter wa Chama cha CHADEMA waliandika kwamba Mjadala wao haukuhusu nafasi ya Mgombea Urais pekeake ila ilikuwepo ishu ya Majimbo 26 ambayo NEC walitangaza kwamba yameongezwa kwenye Uchaguzi mwaka huu.

Magazeti ya leo July 15 2015 yana headlines pia kuhusu stori ya UKAWA kuamua kwamba watamtangaza Mgombea wao ndani ya wiki moja kuanzia sasa.. Ukurasa wa @Twitter wa Gazeti la MWANANCHI wameandika pia mwendelezo wa hiyo stori kuhusu ishu ya Viongozi wa CUF kutoshiriki kwenye Mkutano wa UKAWA jana.

Tweet1 >>>>Mkutano wa na waandishi umeanza hivi sasa katika Makao Makuu ya kuelezea kinachoendelea ndani ya

Tweet2 >>>>: CUF hatukuweza kushiriki katika kikao cha jana kutokana na sababu za kikatiba ndani ya chama ,

Tweet3 >>>>: Maamuzi magumu ya chama huamuliwa na vikao vya maamuzi ndani ya chama, tunaendelea na vikao vya ndani ili kuwa na maamuzi ya pamoja

Tweet4 >>>>: Hatujasusia au kujitoa , hizo taarifa ni za uzushi na uongo, tumeona tuweke mambo ya chama vizuri ili tuende tukiwa wamoja

MWANA MWANANCHI

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments