Duniani

Bibie hakutaka utani, kaamua kutumia Bango kubwa barabarani kutangaza Ndoa imevunjika..

on

Kuna msemo wa Kiswahili unasema,Simulia ila usiombee yakukute !! Pata picha tukio la mpenzi wako analipia kabisa liwekwe Bango kubwa barabarani lenye ujumbe kwamba wewe na yeye biashara yenu imefikia mwisho, yani hakuna mapenzi tena !!

Watu wa maeneo ya Sheffield, Kaskazini mwa Uingereza wameishuhudia hii yani pembeni ya barabara kubwa kabisa, mwanamke mmoja ambaye jina lake ni Lisa aliona afanye maamuzi magumu baada ya kutopendezwa na kitendo cha mumewe kuwa sio mwaminifu kwenye uhusiano wao, mama akaona isiwe shida.. kaenda kwenye Kampuni ambayo inahusika na kuweka mabango makubwa mjini, akalipia na yeye litundikwe Bango lenye ujumbe maalum kabisa kwa mumewe.

MAIN-Sign-on-motorway-woman-dumping-husband

Jamaa nao kwa sababu hiyo ni biashara yao hawakuwa na neno, siku ilipofika wakaenda kutundika Bango hilo ambapo baadhi ya Mashuhuda wamesema walishuhudia Bango hilo linaning’inia kati ya saa 12 mpaka saa tatu asubuhi, muda ambao kunakuwa na msongamano mkubwa wa magari kwa wanaowahi kwenye shughuli zao.

Kwenye Bango kulikuwa na maneno ambayo Lisa aliyaandika kwa mumewe Paul kwamba aendelee tu na maisha yake akirudi hatomkuta nyumbani, na anamtakia kazi njema.

Bango

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments