Duniani

Uko kwenye gari na mtoto wako alafu unavuta Sigara, Uingereza hawakuachii hata kidogo..!!

on

May 24 2015 Tanzania iliungana na Nchi nyingine kuadhimisha siku ya Kifua Kikuu Duniani, kwenye Ripoti za utafiti inaonesha Sigara ni moja ya vitu vinavyochangia tatizo la ugonjwa huo !!

Kwenye Majibu ya Utafiti pia kuna kitu kimegusiwa kwamba wapo wanaopata matatizo ya Ugonjwa wa TB kwa kupatwa na moshi wa Sigara ambayo imevutwa na mtu mwingine… Kuna nchi ambazo tayari walipiga MARUFUKU uvutaji wa Sigara hadharani, kwenye nchi hizo Uingereza na Russia nazo zipo.

sigara3

Ripoti nyingine ni hii toka Uingereza pia… Mara ya kwanza ilikuwa ukikamatwa unavuta Sigara hadharani ni faini au jela au vyote viwili, ikufikie na hii kwamba usidhani ukikamatwa na Sigara yako ndani ya gari alafu umepakia na mtoto wako Sheria itakuacha !!

Sheria hii mpya ina mpango wa kulinda watoto walio chini ya miaka 18, hatari yake ni kwamba moja ya maradhi ambayo anaweza kupata mtoto anayevuta hewa yenye moshi wa Sigara, ni kuugua ugonjwa  wa kansa… Sheria mpya imeruhusu kwa yeyote atakayekamatwa ni faini Pound 50 ambazo ni kama Tshs. 160,000/=.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments