AyoTV

Ukimuliza Ndairagije kwa nini Jonas Mkude hajawasili Taifa Stars, atakujibu hivi

on

Moja kati ya vitu ambavyo vimeendelea kuwa gumzo katika mitandao ya kijamii ni kuhusiana na kiungo wa club ya Simba SC na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Jonas Mkude kutowasili katika kambi ya timu ya taifa ya Tanzania taifa Stars kwa muda uliotakiwa.

Hadi sasa Jonas Mkude hajawasili lakini hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kutokana na kuchelewa kwake, wachezaji pekee wenye ruhusa maalum ya kuchelewa katika kambi ya Taifa Stars ni wachezaji wa Yanga ambao walikuwa mjini Lindi kucheza mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo lakini wachezaji wa Simba SC Aishi Manula, Kapombe na wengineo wamewasili na kuendelea na mazoezi kasoro Mkude.

Kocha mkuu wa Taifa Stars Etienne Ndairagije ameongea na waandishi wa habari mara baada ya mazoezi ya leo jioni ya kujiandaa na CHAN 2020 yaliofanyika uwanja wa Taifa na kusema kuwa hawezi kuongea chochote kuhusu Mkude kutokana na kuwa hana taarifa rasmi  za kuchelewa kwake kambini.

AUDIO: NI KWELI YANGA WANACHEZA VIBAYA KWA SABABU HAWAJAPEWA MILIONI 200 ZAO?

Soma na hizi

Tupia Comments