Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA Dkt. James Andilile, amesema kuwa miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na mamlaka hiyo katika kudhibiti hali ya upatikanaji wa mafuta nchini ni pamoja na kupitia mifumo ya uagizaji na upangaji bei ili kuhakikisha kuna upatikanaji wa mafuta wakati wote.
Dkt. James Andilile ameongeza kuwa pamoja na kuwepo kwa mafuta nchini baadhi ya wafanyabishara wamekuwa wakichukua mafuta na kuchelewesha kufikisha vituoni huku wengine wakiwa na mafuta kwenye visima lakini hawauzi hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi.
Kutokana na ufichaji wa mafuta, Ewura imevichukulia hatua vituo 8 ambavyo vimekuwa na tabia ya kuficha mafuta ambapo tarehe 4 Septemba ilivifungia vituo viwili vya CAMEL OIL Msamvu Morogoro na Matemba Turiani kwa miez