Duniani

Polisi wameinasa selfie ya mtu na mwenzi wake wanaosakwa kwa wizi Uingereza !!

on

Najua inawezekana hata wewe unapenda mkiwa kwenye pozi na mpenzi wako mnapiga zenu selfie, kwa kujiachia kabisa yani.. inakuwaje unaambiwa wewe na mpenzi wako mnatafutwa baada ya kupiga selfie ?!

Kilichowaponza wawili hao na kujikuta wakiingia kwenye mtego wa kusakwa na Polisi ni kwamba, kumbe iPad waliyopigia selfie ni ya wizi, na kosa zaidi ni pale walipopandisha picha hizo kwenye account ya iCloud ambayo imeasajiliwa iPad hiyo… jamaa wa usalama wakawashtukia !!

Polisi wanasema iPad hiyo ni sehemu ya vitu mbalimbali vilivyoibiwa maeneo ya Essex Uingereza usiku wa December 11 kuamkia 12 mwaka 2015…  Polisi wametoa na picha za wawili hao kama kuna yeyote ana taarifa zao atoe taarifa Polisi kwa namba 0800 555111, Uingereza.

Selfie ni nzuri ila kumbe umakini ni kitu muhimu pia, unaweza kujikuta kwenye hatia kama ya aina hii mtu wangu !!

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments