Duniani

Kama unakwepa kuoga ukitegemea perfume, nayo inaweza kukuletea balaa !! Cheki na hii ya Uingereza..

on

Stori inatoka Uingereza ambapo kijana mmoja Thomas Townsend mwenye umri wa miaka 16 amefariki, uchunguzi unaonesha kilichosababisha kifo chake ni matumizi makubwa ya spray za manukato mwilini.

Najua kuna watu wangu wanapenda kunukia vizuri kwa hiyo vitu kama perfume na body spray ni kawaida kwao, naomba niwafikishie na hii kutoka Uingereza.

Kijana huyo Thomas alikutwa akiwa amepoteza fahamu chumbani kwake, baada ya upekuzi Polisi walikuta ndani ya chumba chake kuna makopo 42 ya manukato… na ile harufu yenye gesi kwenye manukato hayo inatajwa kuhusika kusababisha kifo chake.

Mama yake amesimulia pia kwamba mtoto wake hakupenda kuoga, na alikuwa anaweza kupulizia nusu kopo la manukato kwa wakati mmoja !!

Mtaalam mmoja wa masuala ya afya amesema kijana huyo Thomas kafariki kutokana na kuvuta hewa ya gesi ya butane inayowekwa kwenye manukato…!!

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments