Mix

VIDEO: Taarifa ya CHADEMA kuhusu maandamano ya UKUTA ya October 1 2016

on

Baada ya August 31 2016 mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kutangaza kuahirisha mikutano na maandamano ya UKUTA kwa muda wa mwezi ili kuwapa nafasi wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini kutafuta suluhu ya jambo hilo kwa kukutana na Rais Magufuli.

Leo September 30 2016 imebaki siku moja kufika kwa siku iliyotangazwa kama mbadala wa siku ya September 01 2016 ambayo ni October 1 2016, Mwenyekiti wa chama cha maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza kuahirishwa kwa UKUTA…..

>>>’Kamati maalumu ya kamati kuu ya CHADEMA imetambua vilevile kutokana na matukio mengine kadha wa kadha kuwa mapambano ya kisiasa si tukio la siku moja ni tukio endelevu kwa hiyo tarehe moja October iliyokuwa imetangazwa kuwa ni siku mbadala baada ya tathimini mambo kadhaa kamati kuu maalumu imeona kuna umuhimu wa kutokuendelea na maandamo na mikutano nchi nzima iliyokuwa imekusudiwa kufanyika nchi nzima ili kupisha mbinu zingine mbadala‘:-Mbowe

ULIKOSA HII YA CHADEMA KUAHIRISHA UKUTA SEPTEMBER 01 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments