Tayari mfumo mpya wa ulipaji wa ushuru wa maegesho (parking) kwa njia ya kielektroniki umeanza kutumika kuanzia September 01,2021 huku Mtaani kukiwa na malalamiko kadhaa kutokanana na upya wa mfumo huo ambao tofauti na zamani kwa sasa Mmiliki wa Chombo halipii cash bali hulazimika kulipa ushuru kupitia mitandao ya simu, Wakala au kwa njia za kibenki.
AyoTV na millardayo.com zimefika Ofisi za TARURA Mkoani Dar es salaam na kuzungumza na Godfrey Mkinga ambaye ni Mratibu wa Tarura Mkoa wa Dar es Salaam ambaye licha ya kutuelezea namna mfumo huu mpya unavyofanya kazi amewataka Wananchi kupuuza taarifa zinazodai SeriKali kupitia TARURA wameongeza tozo mpya ya maegesho na kusema bei zinazotozwa sasa ni zilezile ambazo walikuwa wanatoza zamani.
“TARURA hatujaja na kitu kipya utaratibu huo unatumika Watu kununua tiketi za Mabasi na za ndege, kulipia umeme, maji n.k lengo ni kuhakikisha mapato ya Serikali yanafika katika Mfuko Mkuu wa Serikali, ukishapark Wakusanya ushuru wakaku-scan unaweza kulipa papohapo kupitia simu yako, wakala au Benki au kama hauna pesa unaweza kuendelea na mambo yako na ukatakiwa kulipa deni ndani ya siku 7, mfumo ni mpya zipo changamoto kwa Wakusanyaji ushuru ila tunaendelea kuwapa mafunzo ili wauelewe baada ya siku kadhaa kila kitu kitakuwa sawa”
“Mmiliki wa chombo anatakiwa kulipia ushuru ndani ya siku 7 akishindwa atapaswa kulipia mara mbili ya anachodaiwa ndani ya siku 14 akishindwa atafikishwa Mahakamani na akitiwa hatiani atalipia faini ya Tsh. Laki 3 au kifunho cha miezi 12 au vyote kwa pamoja, hata hivyo Mhusika endapo atakiri kosa bila usumbufu kanuni itamruhusu Wakala kumtoza Tsh. Elfu 30 baada ya kujaza fomu ya kufifilisha kosa” ———-Mkinga kwenye hii video yumo pia Shadrack Mahenge, Mtaalamu wa Mifumo ya TEHAMA kutoka TARURA akielezea jinsi ya kufanya malipo na kuangalia deni la maegesho kupitia simu yako.
UTACHEKA!! MWIJAKU AKIZICHAPA NA MWAKINYO, ASEMA “IMEINGIA YA TUMBO”