Habari za Mastaa

Ukweli kuhusu Rolls Royce, feki zipo, ya Diamond tofauti yake ‘Service itamtesa’

on

AYO TV na millardayo.com inakukutanisha na Muagizaji magari kutoka UK, Dubai, na Japan iitwayo B-MCAR DEALERS CO.LTD ambapo anatuelezea juu ya gari aina Rolls Royce Cullinan 2021, bei yake kutoka UK na faida pamoja na changamoto zake.

Inategemea kama unahitaji mpya ama iliyotumika pili inategemea umenunulia wapi kwa mfano kwa bei ya Dubai, UK na Singapore ni tofauti tuanze na marketing price ya UK ukihitaji  Rolls Royce mpya inaanzia Pound laki 3 na Elfu 90 kwahiyo unaweza ukajikuta Tanzania unaileta mpaka I.5 Bilioni na hapo haujalipa bado Ushuru’- B-MCAR

Kama ni mpya kabisa basi inaweza ikagusa mpaka Bilioni 2 na hizo zingine zinazo zungumziwa kwamba ni feki kwa Dubai  wana michezo ambayo wanabadilisha labda Injini na vitu vidogo vidogo ila kwa UK hawana huo mchezo’- B-MCAR

Utofauti uliopo ni kwamba ya Rolls Royce na magari mengine ni kwamba sio gari ambalo utaweza kulinunua kwa mtu wa kawaida yale magari wanaendesha matajiri halafu katika upande wa Services itabidi ujipange kwa hali ya juu’- B-MCAR

“UMEBAKI MWEZI MMOJA ITATUA NDEGE YA DIAMOND” – MENEJA WA DIAMOND

Soma na hizi

Tupia Comments